28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Maandalizi ya Mwenge Iramba yakamilika

Na Seif Takaza, Iramba

Zaidi ya Sh bilioni 4 zimetumika kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kijamii wilayani Iramba mkoani Singida katika ujio wa Mwenge wa Uhuru mwaka huu unaotarajiwa kukimbizwa wilayani humo kuanzia Septemba 22, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, mwenge wa uhuru utapokelewa katika Kijiji cha Mseko kitongoji cha Malendi ukitokea Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

Amesema Sh bilioni 4.09 zimetolewa na Serikali Kuu, Sh milioni 39.31 Wahisani, Sh milioni 3.42 jamii na Sh milioni 11.77 Halmashauri ya wilaya ya Iramba.

Mwenda amesema katika kikao cha mwisho cha mwenge wa uhuru kilichofanyika jana katika ukumbi mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kimekamilisha taratibu zote za ujio wa mwenge wa Uhuru wilayani hapa.

Amesema katika Kijiji cha Mseko utazindua mradi wa miti na kufungua shule mpya ya msingi ya Ishenga iliyopo Tarafa ya Shelui na kuzindua Ofisi ya Masjala ya Ardhi katika Kijiji cha Masagi kata ya Mtoa.

Aidha miradi mingine ni mradi wa kikundi cha vijana Chapakazi katika Kijiji cha Mgundu pia utazindua mradi wa utengenezaji Madawati Mugundu na mradi wa Maji katika Kijiji cha Makunda, uzinduzi wa vifaa tiba katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba Kiomboi na utahitimisha kwa kuweka jiwe la Msingi la barabara ya mjini Kiomboi.

‘’Nawaomba watendaji wote viongozi wa Taasisi mbalimbali viongozi wa dini tushiriki kikamilifu katika mapokezi ya mwenge na wote wanaohusika na miradi ya mwenge kuhakikisha nyaraka zote zinakuwepo, nawaombeni msiniangushe ili Wilaya yetu iweze kushinda point zote,” amesema Mwenda huku akisisitia wananchi kujitokeza.

Ujumbe wa Mwenge mwaka huu ni TUNZA MAZINGIRA, OKOA VYANZO VYA MAJI KWA USTAWI WA VIUMBE HAI KWA UCHUMI WA TAIFA’. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles