27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 30, 2024

Contact us: [email protected]

Lulu Diva, Mobetto, Uwoya hapatoshi Uwanja wa Mpaka leo

Brighiter Masaki

MSIMU wa tatu wa tamasha la Nifuate chini ya SamaKiba Foundation, linatarajiwa kufanyika leo katika Uwanja wa Mpaka, Dar es Salaam kwa kuzikutanisha timu Ali Kiba na timu Mbwana Samatta.

Taasisi ya SamaKiba iliundwa miaka mitatu ilioyopita na mchezaji wa Aston Villa ya England, Mbwana Samatta na  Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Kiba, lengo likiwa ni kufanya matukio ya kurudisha kwa jamii.

Kupitia taasisi hiyo ndio tamasha la Nifuate likazaliwa na likajizolea umaarufu mkubwa kwa mchango wake kwenye jamii. Nifuate limekuwa tamasha la michezo na burudani linalowakutanisha watu maarufu kwenye tasnia ya burudani na soka huku mapato yanayopatikana yanapelekwa moja kwa moja kusaidia sekta mbalimbali kama vile afya na elimu.

Mechi ya kwanza ya mchezo wa hisani ulichezwa Juni 1, 2018  ambayo timu inayoundwa na staa wa soka la kulipwa barani Ulaya, Samatta Mbwana, iliibuka na ushindi wa bao 3-1.

Msimu wa pili wa tamasha hilo uliofanyika Juni 11, 2019, ambacho kwenye mechi, Samatta na timu yake waliiendelea kuwa wababe baada ya kuifyatua timu  ya Ali Kiba bao 6-3

Vipi leo hii, nani ataibuka mshindi, je timu Samatta itaendelea kutamba au timu Ali Kiba itapindua meza kibabe kwa kuichapa timu inayoundwa na Mbwana Samatta.

Kivutio kikubwa kwenye tasmasha la Nifuate huwa ni warembo maarufu kutoka kwenye filamu na muziki ambao wao husimama kama mashabiki na kuwapa hamasa wachezaji.

Kwa upande wa Samatta, anawaomba mashabiki wa mpira, wasanii na watu mbalimbali waungane na kushiriki kwenye mchezo huo wa hisani wenye lengo la kusaidia kuchangia elimu bora kwa watoto wa hali ya chini wa Kitanzania

Akaweka wazi baadhi ya wachezaji ambao watakuwa timu yake kuwa ni Mohamed Samatta, Iddy Seleman ‘Nado’, Farid Mussa, Juma Kaseja, Ngasa, Kelvin Yondani, Shomari Kapombe, Deo Kanda huku msemaji wake akiwa ni Haji Manara.

Ali Kiba naye alitangaza kikosi chake ambacho kitakuwa chini ya kocha, Juma Mgunda na msemaji Mwalubadu kuwa ni K2ga, Abdu Kiba, Bakar Mwamnyeto na wengineo kibao ambao watakuwa ‘surprise’ uwanjani.

Katika sekta ya kupamba tamasha hilo, warembo kibao watajitokeza kusapoti mechi kama vile staa wa filamu, Batuli ambaye anasema: “Ninaiunga mkono kampeni ya Nifuate ya Samatta na Ali Kiba na nitakuwepo kwenye Uwanja wa Mkapa kushuhudia.”

Mrembo kutoka Bongo Muvi, Irene Uwoya alisema: “Ninaunga mkono kampeni ya Nifuate na nitakuwepo kwnye mechi hiyo ya hisani.”

Naye Hamisa Mobetto, amewapongeza kwa jambo zuri wanalolifanya kwenye jamii na kuwaunga mkono kwenye mechi ya ili kusaidia watu wenye huhitaji.

Official Nai, amesema yeye ni timu Samatta na anawapongeza kwa kufanya jambo kubwa atakuwepo na atakikisha  timu yake wanaifunga timu Kiba.

Lulu Diva anasena kuwa yeye ni timu Kiba, alisema kati ya Samatta na Ali Kiba yupo kwa Ali Kiba kuwa yeye ameanza kumfatilia muda mrefu kwenye muziki na kucheza mpira na anajuwa uwezo wake, kesho (leo) watawafunga timu Samatta bao tano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles