28.2 C
Dar es Salaam
Monday, July 4, 2022

ALIYEMLETA KAGERE KUSHUSHA ‘MASHINE’ ZA MAANA SIMBA

WINFRIDA MTOI- DAR ES SALAAM

MENEJA wa mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, Patrick Gakumba, amewataka wekundu hao kujiandaa kuwapokea wachezaji wapya wakali kipindi hiki cha usajili.

Gakumba ndiye aliyefanikisha dili la Kagere kutua Msimbazi msimu wa 2018/2019, akitokea Gor Mahia ya Kenya.

Msimu wake wa kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara, Kagere alifunga mabao 23 na kutwaa tuzo ya mfungaji bora, akirudia tena msimu uliopita baada ya kufunga mabao 22

Gakumba, alisema baada ya mteja wake kufanikiwa kuongezea mkataba mwingine wa mwaka mmoja Simba baada ya ule wa awali wa miaka miwili kumalizika, anatarajia kushusha wachezaji wengine wakali.

Alisema hawezi kuwaanika wachezaji hao kwa majina kwa sasa hadi pale watakapokamilisha usajili, kwa sababu suala hilo lipo chini ya uongozi wa klabu hiyo.

“Wapo wachezaji wengine nitawaleta Simba kipindi hiki, mimi huwa sifanyi makosa ya kuchukua wachezaji wasio wazuri, naomba uvumilivu kwa Wanasimba wataona wenyewe,” alisema na kuongeza.

“Kagere tayari ameshamalizana na uongozi wa Simba, tulikaa chini na kuongeza mkataba wa mwaka mmoja kwa fedha  tuliyotaka, ataendelea kuitumikia timu hiyo kwa muda huo,”alisema.

Alisema anaamini wachezaji atakaowaleta  wataisadia Simba katika michuano ya  Ligi ya Mabingwa wanayotarajia kushiriki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,637FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles