31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Shilole, Snura ni ishu ya uchebe au kuna lingine?

Christopher Msekena

ACHANA na uhasama uliupo baina ya Diamond Platnumz na Alikiba au bifu la Konde Boy na mashabiki wa WCB, upande wa wanamuziki wa kike nao hawajacheza mbali. 

Warembo waliopo kwenye Bongo Fleva wamejikuta ndani ya uhasama unaotokana na ishu za muziki huku zikichochewa zaidi na wewe shabiki ambaye hutaki msanii wako aonekane mnyonge mbele ya msanii mwingine. 

Miongoni mwa wasanii ambao inajulikana wapo kwenye uhasama wa muda mrefu ni Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Snura Mushi ambao hawajaanza kuzinguana leo wala jana ila ni kitambo enzi hizo mwaka 2013 wimbo wa Majanga ukisumbua mtaani.

Wawili hao walijikuta ndani ya bifu la ushindani wa kimuziki kwa sababu kipindi Snura anatoka  Shilole naye alikuwa hakamatiki kwenye chati za muziki wa uswahilini na ngoma zake kama Lawama na Dudu.

 Mashabiki walishiriki kuchochea uhasama huo ambao wakeleketwa wa Snura walimpachika jina la Malkia wa Uswazi huku wale wapenzi wa Shishi wakizidi kumwaminia msanii wao na hapo ushindani kati ya wawili hao kwenye muziki ukazidi kuchukua sura mpya.

 Kama unavyojua zinapokutana pande mbili za mahasimu, mashabiki ndio huwa askari wa kwanza kwenye mapambano. Kwa hiyo hata kwenye mvutano huu wa Shishi na Snura, mashabiki ndio walizinguana zaidi kuliko hata wahusika wenyewe.

 Nina uhakika Shilole na Snura hawajawahi kukutana na wakaulizana kama kweli wana bifu au wanachochewa na mashabiki zao. Hawajawahi kuwa washkaji zaidi ya kila mmoja kuwa na historia ya kuhama kwenye tasnia ya filamu na kuingia katika muziki.

Ndio maana wiki hii wawili hao walipoingia kwenye mvutano sikushangaa sana zaidi ya kujiuliza  Shilole na Snura hivi ni kweli vita hii ya maneno imeletwa na ishu ya Uchebe au kuna mengine nyuma ya pazia ambayo mimi na mashabiki hatujui. 

Maana naamini hakukuwa na ulazima wa Shilole kumchoresha Snura kwenye tamasha kubwa kama lile lililokuwa linafuatiliwa na viongozi wakuu wa nchi kwa kusema Snura alifurahia unyanyasaji wa kipigo aliokuwa anapigwa na aliyekuwa mume wake, Ashraf Sadiki a.k.a Uchebe.

Nadhani Shilole alikuwa na haki ya kuongea ya moyoni kuhusu kuchukizwa na Snura lakini sehemu aliyotumia kusemea haikuwa sahihi.

Licha ya Snura kusisitiza kuwa hakuwahi kufurahia kipigo cha Shilole ila alimshauri afuate utaratibu wa dini ya Kiislamu ili kupata haki zake na siyo kuanika mambo ya ndoa yake mtandaoni.

 Naamini kwenye tamasha lile lenye maudhui ya kuwaamsha watoto wa kike katika kuamini na kusimamia ndoto zao hakukuwa na ulazima wa kuingiza ishu za kama hizo ambazo kiukweli ndio zimeteka mtandao na kufunika dhima njema ya jukwaa la Girls Power.

 Watu wameacha kujadili ujasili wa kuigwa wa kusimamia maono aliouonesha Makamu wa Rais, Mama Samia au yule rubani  wa kike, Joanita Bomani kutoka Air Tanzania anayerusha ndege yetu ya Boeing 787 Dreamliner.

Au simulizi za kusisimua zilizojaa ushujaa wa kusimamia maono walionao madaktari bingwa wa kike na yule Profesa wa kike mwenye umri mdogo hapa Bongo, Neema Mori au Editha Kanani ambaye ni dereva na kiongozi wa madareva wa treni jijini Dodoma akiwa mwanamke wa kwanza kwenye Shirika la Reli Tanzania.

Badala jamii hasa wasichana kuwajadili wanawake shupavu walioweza kuvunja ukuta wa vioo unaowatenganisha wanawake na fursa kiasi cha kufikia nafasi za juu kwenye majeshi yetu kama vile, Naibu Kamishna wa Polisi, Mary Nzuki na Brigedia Jenerali Kodi ambaye ni mwanamke pekee mwenye cheo kikubwa kwenye Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), watu wamebaki wakiwazungumzia kina Snura na uhasama wao.

Hii si sawa kwa sababu jukwaa lile halikuwa na lengo la kuibua uhasama bali kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo ya nchi yetu na kutoa hamasa kwa wasichana wadogo kuamini katika ndoto zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles