24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Lugalo Open 2021 kutimua vumbi wiki hii

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

MASHINDANO ya wazi ya gofu ‘Lugalo Open 2021’ yanatarajia kuanza kutimua vumbi Novemba 12-14, 2021 kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu Lugalo, yakishirikisha wachezaji mbalimbali wa kulipwa, ridhaa na vijana ‘Juniors’.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Novemba 10, 2021 klabuni hapo, Meneja wa Klabu ya Gofu Lugalo, Luteni Kanali Frank Kaluwa, amesema muitikio wa wachezaji ni mkubwa  ambapo hadi sasa waliojisajili ni zaidi ya 100.

Luteni Kanali Kaluwa ameeleza kuwa maandalizi yamefanyika vizuri na wadhamini wao Africarries Ltd wamesimama vema kuhakikisha wanafanikisha michuano hiyo.

“Tunatarajia kufanya mashindano ambayo ni makubwa, yanajulikana kama Lugalo Open 2021, tunatarajia yafanyike kuanzia Ijumaa tarehe 12 na kuhitimishwa tarehe 14 Novemba mwaka huu.

“Ni moja ya mashindano ambayo yapo katika ratiba za TGU, ina maana yanasimamiwa na Chama cha Gofu Tanzania na sisi Lugalo tumepewa dhamana ya kuendesha,” amesema.

Amefafanua kuwa wachezaji wa kulipwa wataanza kucheza Ijumaa Novemba 12 -13 Jumamosi 2021.

Amezitaja klabu zitakazoshiriki mashindano hayo kuwa ni mwenyeji Lugalo, Dar es Salaam Gymkhana, Arusha Gymkhana, TPC Moshi, Mufindi Golf Club, Morogoro Gymkhana na Moshi Gymkhana.

Kwa upande wake Mkuu wa Mauzo wa Africarries Ltd, Mohammed Ladha, amesema wameamua kudhamini mchezo wa gofu kwa kutoa fedha sh milioni 30 ili kufanikisha mashindano hayo.

“Safari hii tumependelea kudhamini mchezo huu wa gofu, ni mchezo ambao unajulikana duniani kote, ni mchezo tofauti na mingine, hivyo tukaamua kudhamini kwa kutoa milioni 30 na kufanya vitu vingine,” amesema Ladha.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU), Kanali David Luoga, amewapongeza wadhamini hao kwa kutoa kiasi hicho cha fedha na kuwaomba kuelendelea kufanya hivyo katika mashindano na klabu nyingine.

Pia ameipongeza Klabu ya Lugalo kutokana na kuendeleza mchezo huo hasa kuzalisha vijana wengi  ambapo kwa Tanzania ndiyo inaongoza.

Aidha Nahodha wa klabu hiyo, Meja Japhet Masai amesema mashindano hayo yatafanyika kwa mfumo wa shindano litafanyika kwa mfumo wa mikwaju ya jumla ‘stroke play gross’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles