29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu ‘awasurprise’ Taifa Stars mazoezini

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea mazoezi ya timu ya Taifa, Taifa Stars na kuwaeleza wachezaji kuwa Watanzania wanamatarajio makubwa kwamba timu yao itafuzu na kushiriki kombe la Dunia litakalofanyika, Qatar 2022.

“Nimekuja kuona mwenendo wa mazoezi, matarajio tuliyonayo ni makubwa na tuna imani mtashinda. Mechi ya keshokutwa ni muhimu kwa nchi yetu tunahitaji kushinda mechi zilizobaki ili tutimize malengo yetu. Tunahitaji kuweka historia.”

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati), akishuhudia mazoezi ya Taifa Stars kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam leo Novemba 9,2021, kulia ni Waziri wa Michezo Innocent Bashungwa na Rais wa TFF, Wallace Karia.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Novemba 9, 2021, wakati akizungumza na wachezaji wa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam baada ya kushuhudia mazoezi ya timu hiyo.

Taifa Stars inafanya mazoezi ya kuajiandaa na michezo ya awali ya kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Timu ya Taifa ya DR Congo na Madagascar, ambapo Mheshimiwa Majaliwa amewasisitiza wachezaji wazingatie mafunzo yanayotolewa na walimu.

Waziri Mkuu amesema Serikali kupitia Wizara ya Michezo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wataendelea kuisimamia na kufuatilia maendeleo ya timu hiyo hadi hatua ya mwisho na kuhakikisha inafanya vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles