31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Lugalo mabingwa ‘Amateur Stroke Play’

Na Mwandishi Wetu

MCHEZAJI wa gofu wa  Klabu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Lugalo(JWTZ), Isihaka Daudi ametwaa ubingwa wa mashindano ya Tanzania ‘Amateur Stroke Play’.

Mashindano hayo ya siku tatu yalimalizika Novemba 28,2021 kwenye viwanja vya TPC Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Daudi ambaye aliwapa changamoto wachezaji wenzake, ameshinda kwa mikwaju 210 dhidi ya Ally Mcharo aliyeshika namba mbili kwa 215 huku wa tatu akiwa ni George Sembi aliyepiga mikwaju 218 wote wakitokea TPC.


Mchezaji wa kulipwa Frank Mwinuka mshindi wa kwanza (kushoto) akikabidhiwa zawadi na Prof.  Patrick Ndakidemi  Mbunge wa Moshi Vijijini mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwa mikwaju 143 katika shindano la Tanzania Amateur Strokeplay.
 

Akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo, Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi amevitaka vilabu kuendeleza vipaji vya watoto ili kuongeza chachu ya ushindani Kitaifa na Kimataifa

Kwa upande wake nahodha wa Klabu ya Gofu TPC Jaffari Ally, amezishukuru klabu zote kwa ushirikiano ambao ni bora katika kukuza uhusiano wa klabu za gofu nchini.

Washindi wengine ni divisheni A, mshindi ni Ally Mwinyi kwa mikwaju 209 akimtangulia Jaffari Omary  aliyepiga 215 wote wa TPC.

Mchezaji wa kulipwa Hassan Kadio (kushoto) wa Dar Gymkhana akipokea zawadi kutoka Prof.  Patrick Ndakidemi, baada ya kuibuka mshindi wa pili kwa mikwaju 144 katika shindano la Tanzania Amateur Strokeplay.
 

Divisheni B mshindi wa kwanza ni Peter Gullo kwa mikwaju 136 akifuatiwa na Goodluck Peter 139, huku divisheni C aliyeongoza ni Isaya Kalula alipiga mikwaju  152, wote wa TPC, akifuatiwa na Boni Kiwellu wa Moshi Klabu kwa mikwaju 153.

Kwa upande wa watoto (juniors) mshindi ni John Mwinzani mikwaju 224, akimpiku Ibrahimu Gabriel mikwaju 233 wote wa TPC, wanawake mshindi ni J Daniel wa Kili Gofu mikwaju 138 akifuatiwa na Neema Olomi wa Arusha mikwaju 162.

Wachezaji wa kulipwa mshindi wa kwanza ni Frank Mwinuka kutoka Lugalo mikwaju 143, akifuatiwa na Hassan Kadio wa Dar Gymkhana 144,  nafasi ya tatu ikishikwa na Nuru Mollel wa Arusha kwa mikwaju 146.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles