24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Bata la Dar Leaders Club itameremeta Des 4

Na Mwandishi Wetu

TAMASHA la Bata la Dar, linatarajia kufanyika Desemba 4, 2021, viwanja Leaders Club, lengo kumsapoti  Rais Samia Suluhu Hassan katika kusherekea miaka 60 ya Uhuru  wa Tanzania Bara ikiwa na Rais Mwanamke.

Akizungumza na Mtanzania Digital, leo  Novemba 30,2021 jijini, Mratibu wa tamasha hilo, Steve Mengele, ‘Steve Nyerere’ amesema kuwa tamasha hilo litaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala.

“Tunaenda kuandika kwa kutumia peni ya dhahabu historia ya kuwa na Rais mpambanaji jemedari, Samia Suluhu kwa makubwa anayoyafanya kwa kupenda kufanya maendeleo katika nchi yetu,”

“Viwanja vya Leaders vitaanza kupendeza kuanzia saa 2 :00 asubuhi, kutakuwa na mechi za wilaya kwa wilaya  kwa  soka, mpira wa pete na baadae kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali,” amesema Steve Nyerere.

Ameongeza kuwa wanakwenda  kuifufua Leaders na kuwa mpya, kutoa nafasi kwa wafanyabiashara,mama lishe watakuwa wanauza vyakula kama supu ya utumbo, miguu ya kuku, firigisi na vyakula mbalimbali.

Aidha amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo na kujionea burudani tofauti tofauti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles