23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Lugalo Ladies Open kutimua vumbi kesho

Na Salome Bruno, TUDARCo

Mashindano ya wazi ya gofu kwa wanawake (Lugalo Ladies Open 2021) yanatarajia kutimua vumbi kesho katika viwanja vya Klabu ya Gofu Lugalo, jijini Dar es Salaam.

Lengo la mashindano hayo ni kutafuta wachezaji  watakaounda timu ya Taifa, itakayoshiriki mashindano ya kimataifa ya All Afrika mwaka 2022.

Akizungumzia maandalizi ya mashindano hayo, Ofisa Habari wa Klabu ya Gofu Lugalo, Kapteni Selemani Semunyu, amesema idadi ya wachezaji imefikia 100,  wakiwamo  nyota wa Tanzania.

“Wachezaji nyota wote wanawake Tanzania watakuwepo, mwaka huu mashindano ya  Lugalo Ladies Open yatakuwa na ushindani mkubwa kutokana na aina ya wachezaji wanaoshiriki,” amesema Kapteni Semunyu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Wanawake Tanzania (TLGU), Sofia Vigo, amesema wanashiriki mashindano hayo kwa maandalizi ya kupata wachezaji wa timu ya Taifa.

“Tunaushukuru uongozi wa Lugalo kwa kazi nzuri na kuhakikisha mashindano haya yanafanyika vizuri, watakuwepo wachezaji wengine kutoka Uganda na Kenya,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles