25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe apiga ‘stop’ magari kukamatwa Shinyanga

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

NAIBU  Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema Mkoa wa Shinyanga unakiuka maelekezo ya wizara yake  kukamata magari yanayobeba mazao ya dengu ,kunde na mbaazi hivyo amemtaka Mkuu wa Mkoa huo,Dk. Philemon Sengati  kuacha zoezi hilo  mara moja.

Hatua hiyo  imetokana na zaidi ya magari 30 yaliyokuwa yamebeba zao la dengu kuzuiliwa mkoani humo kwa madai ya kukiuka masharti ya stakabadhi ghalani.

Bashe ametoa maagizo hayo leo Agosti 27,2021, jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuanzia sasa magari yote yaliyokamatwa katika mkoa wa Shinyanga yaachiwe mara moja.

Amesemakitendo hicho kinachofanywa na uongozi  wa mkoa wa Shinyanga ni cha kibabe.

Amesema kuwa wafanyabiashara wana leseni lakini wanapofika katika Shinyanga wanakamatwa  wakati mwenye  mamlaka ya kuagiza zao liuzwe kwa namna gani katika minada ni waziri wa kilimo pekee.

“Jambo hili haliwezekani,wafanyabiashara wamelipa ushuru  lakini wanakamatwa,hatutaki namna hii jambo hili sio zuri,”amesema.

Hata hivyo ,Bashe amesema  hali hiyo haitajirudia Shinyanga huku akiwapa pole wakulima pamoja na wafanyabiashara waliopata kadhia hiyo.

“Niwahakikishie wakulima na wafanyabiashara wa nchi hii wizara ya kilimo itaendeelea kuwalinda kwa nguvu zote kuhakikisha mazingira ya kufanya biashara yanakuwa rafiki,”amesema Bashe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles