25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Kalima afikisha salamu za Rais Samia Kasulu

Na Salome Bruno, TUDARCo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Gilbert Kalima, amefanya ziara katika Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma na kutembelea shule ya sekondari Kasulu.

Kalima ameongozana na Mkuu wa Kitengo cha Milki kutoka Makao Makuu ya CCM, William Obimbo na Mwanasheria wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Wakili Beatus Mafuru.

Katika ziara hiyo amekutana nana Kamati ya Siasa ya Wilaya, Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi ya wilayani, bodi na uongozi wa shule, watumishi na wanafunzi.

Katibu huyo amewakumbusha viongozi na wanachama kuwa chama na jumuiya zake kinaendesha mambo yake kupitia vikao na sio mahali pengine huku akiwasisitiza  kufanya vikao visivyo rasmi ni kwenda kinyume na kanuni na sheria za CCM na jumuiya.

Aidha amefikisha salamu za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Rais, Samia Suluhu Hassan, na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Dk.Edmund Mndolwa.

“Ningependa kufikisha salamu kwa viongozi na wanachama na kipekee kwa wanafunzi wa Kasulu na uongozi wake kwa ujumla kwa kazi nzuri wanayofanya kiasi cha kupata matokeo mazuri sana katika mtihani wa kidato cha sita mwaka huu,” amesema Kalima.

Pia amewataka kuendelea kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM 2020 – 2025 kama sehemu ya wajibu mama wa Chama.

Katika hatua nyingine amehimiza umuhimu wa kutoa elimu kwa wananchi na wanachama juu ya chanjo ya Uviko 19 na elimu juu ya tozo mbalimbali mpya zilizoanzishwa na serikali kwa lengo la kusukuma maendeleo ya watu katika maeneo ya barabara za vijijini, elimu, umeme na afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles