24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

LISSU: CASTRO MWAMBA WA SIASA DUNIANI

 JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM


 

fidel-castroMWANASHERIA Mkuu za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, amemwelezea Rais wa zamani wa Cuba, marehemu Fidel Castro kama mmoja wa miamba mikubwa ya siasa za dunia.

Katika taarifa aliyoituma katika mitandao ya jamii jana, Lissu alimwelezea Castro kuwa ni mmoja wa miamba mikubwa ya siasa za nchi zinazoendelea na katika nusu ya pili ya karne ya 20 ametoa pumzi yake ya mwisho.

“Henry Kissinger, Mwanadiplomasia wa Marekani na hasimu mkubwa wa Mapinduzi ya Cuba chini ya Fidel (Castro), aliwahi kumwita ‘the most consistent revolutionary alive’ hatunaye tena. Mshindi wa Cuito Cuanavale na mkombozi wa Namibia, Afrika Kusini na mlinzi wa uhuru wa Angola amepumzika.

“Tutamkumbuka kwa mengi: Cuba ya Castro imefundisha wanafunzi wengi zaidi wa nchi zinazoendelea katika fani mbalimbali kuliko mataifa mengi makubwa na tajiri,”aliandika Lissu.

Alisema Cuba ilifanya hivyo bila kudai malipo yoyote wala kutaka kudhibiti na kunyonya rasilmali za nchi hizo.

“Cuba ya Castro imepeleka madaktari na wafanyakazi wengi wa afya katika nchi masikini kuliko nchi nyingine yoyote. Mwaka ‘1975 na baadaye mwaka ‘1988 ilituma maelfu ya askari wake kwenda kutetea uhuru wa Angola dhidi ya mashambulio ya makaburu na marafiki zao wa kibeberu wa Magharibi.

“Quifangondo, Ebo, Tchipa na Cuito Cuanavale ni majina ambayo yatakuwa ‘yanahusishwa’  na Cuba kwa vizazi vingi vijavyo. Pia Cuba ya Castro ilipigania uhuru wa Algeria, Guinea Bissau na Congo ya Lumumba, Ethiopia (Ogaden) na hata Syria baada ya ‘Six Day War’.

Alisema licha ya mataifa makubwa ya Magharibi na pengine Urusi, Cuba ilikuwa nchi pekee kufanya programu ya ‘military power’ nje ya bara lake ili kutetea uhuru wa nchi hizo.

Castro aliyaita mapambano dhidi ya ‘ubaguzi wa rangi Afrika Kusini katika njia nzuri zaidi…’

“Go thee well Commandante en Jefe. Rest in peace the Victor of Quifangondo and of Cuito Cuanavale. Adieu Fidel Alejandro Castro Ruz’,”aliandika Lissu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles