32.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Lipumba aapa kutoshiriki uchaguzi, kupigania Tume Huru

Mwandishi Wetu, Dar es salaam

MWENYEKITI wa chama cha upinzani cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema chama chake hakitashiriki tena uchaguzi nchini humo mpaka Tume Huru ya uchaguzi iundwe.

Profesa Lipumba alisema hakubaliani na matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 28, kwa kuwa umegubikwa na mapungufu.

“Zoezi la kuwaapisha mawakala liliendeshwa kinyume cha taratibu, uchaguzi wa mwaka huu haukuwa na siri, kwa sababu kwenye karatasi za kupiga kura ziko namba za vitambulisho vya wapiga kura,” alisema.

Alisema CUF imefikia maazimio ya kuhamasisha wananchi na wadau wengine kudai Katiba Mpya yenye misingi ya demokrasia na utawala bora.

Alisema chama hicho kinaomba wanachama na Watanzania kwa ujumla kufunga kula chakula cha mchana siku ya Alhamis na kufanya Dua kila mmoja na imani yake kumuomba Mungu hukumu ya haki kwa kilichotokea katika uchaguzi mkuuwa mwaka huu.

Alisema suala la ujenzi wa demokrasia ni suala linalowahusu Watanzania wote na kwamba Tanzania siyo kisiwa cha kpekee, kwa kwua hata wakati wa kupigania uhuru chama cha Tanu kilikuwa na mahusiano na Labour Party ya Uingereza, chama ambacho kilikuwa ndani ya bunge.

Alisema chama hicho kilikuwa na mahusiano ia na wabunge ambapo hata mama Joan Wicken ambaye alikuwa Katibu Muhtasi wa Mwalimu Julius Nyerere tangu mwaka 1960 hadi mwalimu anafasriki alitoka kwenye Fabian Society ya Uingereza ambapo pia ilikuwa na uhusiano na chama cha Labour.

Lipumba alisema chama cha Tanu pia kilikuwa na mahusiano na chama cha Congress cha India ambayoilikuwa imeshapata uhuru kwa hiyo Tanzania ilishiriki sana kwenye masuala ya Umoja wa Mataifa (UN) ambapo Mwalimu Nyererw alikwenda UN mara kadhaa kwa ajili ya kudai Uhuru wa Tanganyika kwa muda mrefu.

Alisema katika amsuala ya kudai haki ambapopia kuna jumuiya ya kimataifa inaweza kushirikishwa lakini watakaoleta haki na demokrasia nchini si watu wan je, bali ni wananchi wenyewe wa Tanzania.

Alisema kwa chama chake hakitamzuia mbunge wake pekee aliyefanikiwa kushinda ubunge kushiriki katika shughuli za Bunge la Jamhuri.

Aliongeza kusema CUF itaaanzisha mazungumzo na Jumuiya ya Kimataifa kuhusiana na suala hili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles