26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Lampard: bila Hazard kazi tunayo

CHELSEA, ENGLAND

KOCHA mpya wa timu ya Chelsea, Frank Lampard, ameweka wazi kuwa, kuondoka kwa kiungo wao mshambuliaji Eden Hazard kumeiacha timu hiyo kwenye wakati mgumu.

Hazard alikuwa mmoja kati ya wachezaji wenye mchango mkubwa wa mafanikio ya Chelsea kwa kipindi cha miaka saba iliopita, lakini wakati huu wa kiangazi amejiunga na mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid.

Msimu uliopita wa Ligi Kuu England mchezaji huyo alihusika kwenye mabao 31 ya timu hiyo huku mwenyewe akifunga mabao 16 na kutoa pasi 15 za mwisho, lakini kuondoka kwake kumeifanya klabu hiyo ishindwe kumpata mchezaji ambaye anaweza kuziba nafasi hiyo.

Baada ya Chelsea kuanza vibaya katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Manchester United kwa kuchapwa mabao 4-0 mwishoni mwa wiki iliopita, kocha Lampard amedai ni vigumu kuziba nafasi ya Hazard kwa mchezaji mmoja.

“Nilikuwa shabiki mkubwa wa Eden Hazard nikiwa kama shabiki wa Chelsea, hata hivyo nilicheza na yeye pamoja, kwa upande wangu niweke wazi ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani kutokana na kile alichokifanya akiwa Chelsea.

“Alikuwa kama kiongozi ndani ya timu, alikuwa anafunga mabao pamoja na kutoa pasi nyingi za mabao, vigumu sana kuziba nafasi ya mchezaji huyo kwa mchezaji mmoja kwa kuwa alikuwa kwenye kiwango cha hali ya juu.

“Lakini tunatakiwa kutulia na kuwa wavumilivu kutokana na hali hiyo, tuna kundi kubwa la wachezaji, wengine ni chipukizi na wengine ni wazoefu, hivyo ni wakati wao sasa wa kuonesha uwezo wao.

“Hii sio mara ya kwanza kwa Chelsea kumpoteza mchezaji mwenye uwezo mkubwa kama Hazard, aliwahi kuwepo John Terry, Didier Drogba na wengine wengi, lakini waliondoka na timu ikawa inaendelea vizuri,” alisema kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles