Bern, Uswisi
Aliyewahi kuwa Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa (UN), Koffi Anan ameaga dunia mapema leo asubuhi leo akiwa na umri wa miaka 80 baada ya kuugua kwa muda mfupi, Taasisi yake imethibitisha kupitia ukurasa wao wa Twitter.
Annan alikuwa Mwafrika wa kwanza mweusi kuchaguliwa kuwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alizaliwa mwaka 1938 huko Kumasi nchini Ghana, aliitumikia UN kwa mihula miwili kuanzia mwaka 1997 hadi 2006 na aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel.
“Ni huzuni kubwa kuwa familia ya Annan na Taasisi yake ya ‘Koffi Anann Foundation’ kutangaza kuwa aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Koffi Anan amefariki dunia leo Agosti 18, baada ya kuugua kwa muda mfupi,” imeandika Taasisi ya Kofi Annan.
Annan ameacha mke na watoto watatu.