24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

MABINGWA WA MIFUPA CHINA WASAINI MKATABA NA MOI

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM


TAASISI ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imesaini mkataba wa ushirikiano kati yake  na hospitali ya kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing, nchini China.

Akizungumza na MTANZANIA ofisini kwake jana, Ofisa Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi alisema mkataba huo utajikita katika eneo ya tiba, utafiti na mafunzo.

Alisema mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk. Respicious Boniface pamoja na Rais wa Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking, Ms Hongxia Yu.

“MOI itanufaika katika kuboresha huduma za kibingwa za daraja la juu (super specialised services) katika maeneo ya upasuaji wa mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu,” alisema.

Mvungi alisema hafla ya kusaini mkataba huo imeshuhudiwa pia na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki na Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Muhamed Kambi.

Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya Waziri Ummy, ambaye yuko kwenye ziara ya kikazi nchini China kufanya kikao na Rais wa Hospitali ya kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking jijini Beijing, kuhusiana na kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za tiba za kibingwa hapa nchini.

“Hospitali ya kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking ina uzoefu mkubwa katika matibabu ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu, ambapo ina vitanda 1,800 vya kulaza wagonjwa, ICU vitanda 171, Vyumba vya upasuaji 48 na kwa mwaka inahudumia zaidi ya wagonjwa milioni 14.7,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,051FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles