23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha: Arsenal, Tottenham hazinitishi

LONDON, England

KOCHA wa Sunderland, Lee Johnson, amesema hahofii kukutana na Arsenal wala Tottenham kwani timu hizo za Kaskazini mwa London si kubwa kama inavyoonekana.

Sunderland wanasubiri droo ya robo fainali ya Kombe la Ligi (Carabao Cup) itakayochezeshwa wikiendi hii na ni baada ya kuifunga QPR kwa penalti 3-1 baada ya matokeo ya kutofungana.

“Ningependa kwenda ugenini kukutana na Arsenal au Tottenham, au timu nyingine kama hizo,” amesema Lee, ambaye Sunderland yake imeingia robo kwa mara ya kwanza tangu ilipokanyaga hatua hii msimu wa 2013-14.

Ifahamike kuwa Arsenal walitia mguu hatua hii kwa kuitandika Leeds United mabao 2-0, huku Spurs wakitafuta hatima yao katika mchezo wa leo dhidi ya Burnley.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles