23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Fifa ‘yamtungua’ kocha Nigeria

LAGOS, Nigeria

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemfungia miaka miwili kujihusisha na mchezo huo kocha wa Cofine FC inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu nchini Nigeria, Remi Amadi.

Adhabu hiyo ya FIFA imekuja baada ya Amadi kukiri mbele ya Kamati ya Shirikisho la Soka Nigeria (NFF) kuwa alijaribu kupanga matokeo katika mchezo kati ya timu yake na Bussdor FC.

Taarifa ya kufungiwa kwake imewekwa hadharani na NFF jana, ikikumbukwa kuwa Amadi alifanya ‘uhuni’ huo miezi saba iliyopita.

Awali, Kamati ya Nidhamu ya NFF ilishamshushia rungu la kifungo cha kutojihusisha na kandanda kwa miaka miwili, pia klabu yake ya Cofine FC ikatozwa faini ya Naira 500,000 (zaidi ya Sh mil. 2 za Tanzania).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles