KOCHA wa timu ya taifa ya Angola, Pedro Gonçalves, amesema kukosekana kwa wachezaji wake 15 kumechangia kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Misri katika mchezo wa jana wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwakani.
Kama ilivyo kwa Misri iliyocheza bila Mohamed Salah, Angola nayo iliwakosa nyota hao kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo watano waliobainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.
“Hata maandalizi yalikuwa hovyo, timu ilichelewa kuingia kambini. Unakutana na timu ngumu kama Misri, lazima itakuwa ngumu kushinda,” amesema.
Aidha, Goncalves anaamini Angola ingeweza kuambulia sare katika mechi hiyo endapo kikosi chake kingekuwa kimekamilika.