22.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kobe Bryant kustaafu kikapu leo

Kobe-Bryant-5LOS ANGELES, MAREKANI

NYOTA wa kikapu wa timu ya Los Angeles Lakers, ambayo inashiriki Ligi ya Kikapu nchini Marekani, Kobe Bryant, leo hii anatarajia kutangaza rasmi kustaafu mchezo huo baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Utah Jazz.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37, amekuwa katika klabu hiyo kwa miaka 20 na kuisaidia kutwaa mataji mbalimbali na kumfanya kuwa katika orodha ya wachezaji bora duniani kwenye mchezo huo.

Kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Utah Jazz, mchezaji huyo amefanikiwa kujikusanyia pointi 33, 570 na kuwa kati ya wachezaji watatu duniani ambao wamekuwa na alama nyingi katika kipindi chao cha mchezo huo.

Maelfu ya mashabiki walijitokeza katika mchezo huo kwa ajili ya kumuaga nyota huyo, baadhi yao wakiwa wamevaa jezi ya mchezaji huyo.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, mwanzoni kwa wiki hii mchezaji huyo aliweka wazi kwamba katika mchezo dhidi ya Utah Jazz utakuwa ni mchezo wake wa mwisho katika kikapu.

“Muda wangu wa kuwaaga mashabiki na wadau wote wa mchezo wa kikapu umefika, nashukuru kwa ushirikiano wote, nawapenda sana,” aliandika Bryant.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles