28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Ancelotti: Waamuzi hawana mchango kwa Barcelona

Carlo AncelottiBARCELONA, HISPANIA

KOCHA wa zamani wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, ameweka wazi kwamba klabu ya Barcelona haibebwi na waamuzi kama baadhi ya wachezaji wanavyolalamika.

Wiki iliyopita katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali ya kwanza, Barcelona ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Atletico Madrid, mshambuliaji wa Atletico, Fernando Torres, alioneshwa kadi nyekundu na kudai kwamba Barcelona inabebwa na waamuzi.

Hata hivyo, beki wa klabu hiyo, Filipe Luis, naye alisema kwamba bila Barcelona kubebwa Chama cha Soka Ulaya ‘UEFA’ kitakuwa na wakati mgumu.

Ancelotti ameamua kujibu kauli za wachezaji hao na kudai kwamba ushindi wa klabu hiyo unatokana na uwezo wa wachezaji wake wenyewe.

“Sio kwa ubora huu wa Barcelona ya sasa, waamuzi wana uwezo mkubwa sana lakini kuna wakati wanafanya makosa madogo madogo, ninajitahidi kuheshimu uwezo wa waamuzi wetu na hakuna ukweli wowote wa waamuzi kuwabeba Barcelona.

“Nakumbuka miaka mitatu iliyopita, PSG walicheza vizuri dhidi ya Barcelona katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini baada ya kuingia Lionel Messi mambo yalikuwa magumu kwa PSG kwa kuwa mchezaji huyo aliubadilisha mchezo kwa kiasi kikubwa na mashabiki walitoa mchango wa kusapoti.

“Barcelona ya sasa ni hatari sana hasa katika safu ya ushambuliaji ya Messi, Suarez na Neymar, unatakiwa kuwa makini kupambana na wachezaji hao kwa kuwa kila mmoja analijua goli,” alisema Ancelotti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles