23.4 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Ronaldo: Hata nikizomewa nitaendelea kuwa bora

FC Barcelona v Real Madrid CF - La LigaMADRID, HISPANIA

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ameweka wazi kwamba hata kama kuna watu wanamzomea akiwa uwanjani lakini bado ataendelea kuwa bora.

Mchezaji huyo juzi alionesha uwezo wake na kuisaidia klabu hiyo kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo aliifungia mabao matatu katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Wolfsburg.

Katika mchezo wa awali, Madrid ikiwa ugenini nchini Ujerumani dhidi ya wapinzani hao, ilipokea kichapo cha mabao 2-0, hivyo katika mchezo wa jana walitakiwa kushinda ushindi huo ili kusonga mbele.

“Nimekuwa na kipindi kigumu sana msimu huu hasa kwa baadhi ya mashabiki wangu, lakini kuzomea kwao wala hakusaidii lolote na nitaendelea kuwa bora.

“Nimekuwa nikijituma kwa ajili ya kupunguza maneno yao na ninaamini ninaisaidia timu kwa kiasi kikubwa kutokana na ushirikiano ninaoupata kutoka kwa wachezaji wenzangu.

“Kufunga mabao matatu haina maana kwamba uwezo wangu umeishia pale, kila siku nakuwa na lengo la kufunga mabao mengi kwa ajili ya manufaa ya timu na nitaendelea kujituma bila ya kujali watu wanasema nini na ninaamini nipo katika timu bora duniani,” alisema Ronaldo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles