Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital
KITENDO cha kupata kuifunga Azam FC katika mchezo uliopita, kimeipa jeuri KMC FC baada ya kutamba kuendeleza ubabe kesho Novemba 27,2021 itakapoikabili Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.
Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakuwa was aba kwa KMC ambayo kati ya michezo sita imepata ushindi mechi moja ambayo waliifunga Azam mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, huku ikitoka sare miwili na ikipoteza mitatu.
Kwa upande wa Mbeya City haijapoteza mechi katika michezo sita iliyoshuka dimbani ikishinda miwili na sare nne na kukaa.
Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Kocha Msaidizi wa KMC, Habib Kondo, amesema walijiandaa tangu Dar es Salama, Mbeya wamekwenda kupigania pointi tatu.
Ameeleza kuwa wanafahamu wanakutana na timu nzuri ambayo haijapoteza mchezo lakini anajua soka halichezwi kwa historia chochote kinaweza kutokea.
“Tuko na kikosi kamili, tumekuja kupambania pointi tatu, tumeshashinda mechi moja tunataka kushinda nyingine,” amesema Kondo.