26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

KMC mambo magumu yapigwa nyumbani

Na Mwandishi Wetu

TIMU ya Manispaa ya Kinondoni, KMC mambo yameendelea kuwa magumu baada ya kukosa ushindi katika mchezo wa tano mfululizo kwa kufungwa na Kagera Suga bao 1-0 kwenye  Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa leo  Oktoba 29,2021, bao  pekee la Kagera Sugar  limefungwa na Meshack Abraham dakika ya 17.

Baada ya mchezo huo, wachezaji wa KMC walionekana wakisononeka baadhi yao akiwamo kipa Farouk Shikalilo wakikaa chini na kuzunika.

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulivyo baada ya mechi za leo Oktoba 29,2021

Kocha Msaidizi wa KMC, Ahmady Ally, amezungumzia mchezo huo na kusema wamepoteza kutokana na kukosa umakini na wapinzani wao kutumia nafasi hiyo na kukiri kuwa wanahitaji kuongeza nguvu.

“Hatuko vizuri kwa kweli, tunatakiwa kujiangalia na muda huu wa mapunziko  inatakiwa kujipanga kujirekebisha kwa sababu ligi ni ngumu,” amesema Ally.

Mchezo mwingine wa leo uliikutanisha Mbeya Kwanza na Biashara United ambao walitoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles