24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

‘Dar Boxing Derby’ yaiva mabondia wapima uzito

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

JUMLA ya mapambano 14 yanatarajia kupigwa kesho Oktoba 30, 2021 katika usiku wa ‘Dar Boxing Derby’ ambapo leo Oktoba 29,2021 mabondia wamejitokeza kupima uzito wakishuhudiwa na mashabiki waliofurika kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam.

Mapambano makubwa yatamkutanisha Francis Miyeyusho dhidi ya Adam Kipenga na Iddi Piarali atatwangana na Ramadhan Shauri.

Aidha Selemani Kidunda atachapana na Jacob Maganga  kupigania  ubingwa wa Taifa wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) uzito wa ‘super middle’.

Selemani Kidunda(Kulia) na Jacob Maganga(Kushoto), wakitunishiana misuli wakati wa kupima uzito leo kwenye Uwanja wa Kinesi.

Pambano mengine yenye ushindani ni kati ya Grace Mwakamele na Asha Ngedele, Ismail Galiatano dhidi ya Allan Kamote, George Bonabucha atapigana na Haji Juma.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Miyeyusho amesema ataendeleza ubabe wa kuwapiga mabondia wote wa Mabibo na Manzese, huku Kibenga akitamba  kuzima ngebe za mpinzani wake huyo.

Iddi Piarali (kushoto) na Ramashani Shauri(kulia), wakitunishiana misuli

“Ninachoomba tu kesho Adam Kipenga awahi uwanjani nimuoneshe kwa sababu leo siku ya kupima uzito tu  kakimbia amechelwa, asije akakimbia,” ametamba Miyeyusho.

“Mimi nimechelewa kwa sababu nilikuwa nafanyia mazoezi Afrika Kusini nimetua leo saa tano na ndenge, foleni ikanichelewesha, siogopi wala nini nampiga mapema tu Miyeyusho. Tumechoka dharau watu wa Mabibo,” amesema Kipenga.

Asha Ngedele (kushoto), Grace Mwakamele(kulia) wakitambiana, katikati ni kocha wa ngumi Super D.

Naye Kidunda ameahidi kupeleka mkanda jeshini, kwani atahakikisha anampiga Maganga kwa TKO.

“Mimi ni mtu mbaya wote wananijua, nimejiandaa vizuri, nitampiga vibaya Jacob Maganga,siongei sana watu waje Kinesi kuona ngumi,” ametamba Kidunda.

Kwa upande wake Promota wa mchezo huo, Kapteni Selemani Semunyu, amewataka mashabiki kufika mapema kwa sababu wataweka pia TV kubwa ili wale mashabiki wa soka kushuhudia mechi ya Yanga na Azam.

Ismail Galiatano(kulia), Allan Kamote (kushoto), wakitambulishwa kwa mashabiki baada ya kupima uzito na Promota wa mchezo huo Kapteni Selemani Semunyu kwenye Uwanja wa Kinesi leo.

“Mapambano yataanza mapema, saa 12:00 jioni, ulinzi upo wa kutosha, pia mashabiki wa soka tutawafungia screen kubwa kuangalia mechi ya kesho, huku wakishudia ndondi,” amesema Kapteni Semunyu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles