29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Kizimbani akidaiwa kumtukana Rais

Rais John MagufuliNa Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

MAHAKAMA Ya Hakimu Mkazi Kisutu imempandisha kizimbani, Leornard Kyaruzi kwa mashitaka mawili ya kumtukana na kumdhalilisha Rais John Magufuli.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu, Magreth Bankika, Wakili wa serikali, Simon Wankyo alidai   mshtakiwa   alitenda kosa hilo kwa kutumia simu ya mkononi kwenye mtandao wa  jamii wa’ Whatsapp’.

Alidai kuwa  Juni 2, 2016 kwenye mtaa wa Tanzanite Tower  barabara ya Bagamoyo  Dar es Salaam,  mshtakiwa   alitumia simu ya mkononi na kuandika ujumbe wa maneno.

Alidai  ujumbe huo ulikuwa unasomeka: “Hivi huyu Pombe ni kwamba hana washauri? Hashauriki? au ni zuzu! Bwege huyu jamaa, he doesn’t consider the law in place before opening his mouth! Au na yeye anaumwa ugonjwa wa Mnyika?”

Mwendesha mashitaka alidai kuwa shtaka la pili  la mshtakiwa huyo ni   kusambaza ujumbe huo wa kumdhalilisha kiongozi huyo kwenye mtandao huo.

Alisema  upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuiomba mahakama hiyo kuwapa siku 28  waweze kufanya upelelezi wa kina ikiwa ni pamoja na kuangalia maeneo ambayo yanahitajika zaidi kwenye kesi hiyo.

Hakimu Bankika alimtaka mshtakiwa   kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh milioni moja.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana mashitaka na kutolewa nje  dhamana baada ya kukidhi masharti ya dhamana.

Hakimu Bankika aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 18 mwaka huu itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles