23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mhariri kortini kwa kifaru cha jeshi

Pg 3Na Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewapandisha kizimbani, mhariri na mwandishi wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Musa Mkama na Prince Newton wakidaiwa kuandika habari za uongo zilizoleta mtafaruku kwa jamii.

Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Respicius Mwijage, Mawakili wa serikali, Timon Vitalis na Hellen Mushi, walidai     Juni 20 katika eneo la Biafra Kinondoni,  Dar es Salaam, washtakiwa  waliandika na kuchapisha habari za uongo katika gazeti la ‘Dira ya Mtanzania’ toleo la 424 la tarehe 20 hadi 26 ambazo zilisababisha hofu na mshtuko kwa jamii kwa kutoa taarifa za uongo kuwa ‘Kifaru cha kivita cha Jeshi la Wananchi(JWTZ), chaibwa’.

Alidai  kitendo hicho ni kosa katika sheria na ni kinyume na sheria ya magazeti.

Wakili Vitalis alidai   upelelezi wa kesi hiyo  unaendelea na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine   ya kutajwa.

Hata hivyo, washtakiwa hao walikana shtaka hilo na Hakimu Mwijage aliwataka kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh milioni tano.

Washtakiwa hao walikidhi masharti ya dhamana na Hakimu Mwijage aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 5 mwaka huu itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles