21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kiwanda cha Sukari Kilombero kusaidia ajira kwa wahitimu

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Uhakika wa ajira imekuwa ni changamoto kubwa inayowakabili vijana wengi wanaohitimu kwenye vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini.

Hatua hiyo imekuwa ikipelekea wahitimu wengi kuzunguka huku na kule wakiwa pamoja na bahasha zao kusaka ajira huku wengine wakifuatilia nafasi za kazi kwenye magazeti ya kila siku kuona iwapo wanaweza kubahatisha kwenye matangazo hayo yanyowekwa kwenye machapisho hayo.

Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa mengi ya matangazo hayo yamekuwa yakiweka sharti kwa waombaji wa kazi kuwa na uzoefu wa miaka kadhaa hatua ambayo imekuwa kiunzi kwa wahitimu wengi kufuzu kigezo hicho cha kupata ajira kupitia matangazo hayo.

Changamoto hiyo na nyingine ndiyo iliyokisukuma Kiwanda cha Sukari Kilombero kwa kushirikiana na chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Ndaki ya Kilimo kuanzisha mpango wa kutoa nafasi kwa wanafunzi wa ndaki hiyo kupata mafunzo kwa vitendo mahala pa kazi ili wapate ujuzi na uzoefu.

Meneja rasilimali watu wa kampuni ya sukari Kilombero, Beda Chacha amesema mbali na kutoa nafasi ya kujifunza kwa vitendo kampuni imeanzisha programu ya “Bursary scheme” ambapo kiwanda cha sukari kilombero kinatoa ufadhiri wa masomo kwa wanafunzi na kuwaajiri ili kuleta ufanisi wa kiwanda kupata kupata wafanyakazi wenye weredi katika kutimiza majuku yao.
 
Chacha amesema mpango huo umewezesha vijana 53 kuweza kupata mafunzo kwa vitendo na ufadhili wa masomo ambao uliwawezesha wahitimu kuajiliwa na kiwanda.

Ras wa ndaki ya kilimo SUA, Prof Bernard Chove amesema yapo mafanikio mengi waliopata ndaki baada ya kuingia makubaliano ya kupeleka wanachuo kufanya mazoezi ya vitendo katika kiwanda cha sukari kilombero katika kuwasaidia wahitimu kuhitimisha masomo yako kwa kiwango kinachostahili.

Prof. Chove amekipongeza kiwanda cha sukari kilombero huku akitoa mfano wa wahitimu kuajiliwa na kiwanda hicho pindi wanapomaliza chuo na wengine kupata ufadhili wa kila kitu ikiwemo ada.

Aidha, Prof. Chove ametoa wito kwa viwanda vingine kuiga mfano wa kiwanda cha sukari kilombero katika kupokea wahitimu waweze  kujifunza kwa vitendo na kutoa ufadhili  kwa wanafunzi.

“Niliwapeleka wanafunzi wa mwaka wa tatu kufanya mazoezi ya vitendo kiwanda cha  kilombero lakini baadae baadhi ya wahitimu hao walipata ufadhili wa kulipiwa kila kitu na kiwanda kwa mwaka wa nne na kuajiliwa kabisa huku wakiendelea kumalizia masomo yao,” amesema Prof. Chove.

Tumaini Sawe ni Muhitimu wa shahada ya kwanza ya Uhandisi Kilimo chuo kikuu cha sua ndaki ya kilimo mwaka 2020 analeza jinsi kiwanda cha sukari kilivyomsaidia ufadhili wa masomo katika mwaka wan ne na kupatiwa ajira baada ya kufanya vizuri alipoenda kiwandani hapo kufanya mazoezi ya vitendo kupitia makubaliano baiana ya kiwanda cha sukari  kilombero na ndaki ya SUA.

Tumaini ambaye alitoka katika shule za kawaida za serikali kabla ya kujiunga na SUA anasema amesoma elimu ya msingi shule ya Mazimbu A mkaoni Morogoro na kidato cha nne amemaliza sekondali ya Kihonda huku  kidato cha sita amemaliza sekondari ya wasichana Bwiru ilipo mkoani Mwanza.
 
Mwingine ambaye amenufaika na mpango huo wa “bursary scheme” ni Shukuru Thomas ambapo baada ya kwenda kufanya mazoezi ya vitendo kwa mwaka wa tatu aliweza kupata ufadhili wa kila kitu mwaka wanne  na kuajiliwa kabisa  na kiwanda cha sukari kilombero huku akiwa mwananfunzi anaendaliwa na kuifahamu vizuri kampuni ya kilombero.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles