31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Shirika la Bayer kutumia Sh bilioni 1.2 kuwasaidia mbegu wakulima

Na Janeth Mushi, Arusha

Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na sayansi ya kilimo katika nyanda za afya na lishe bora la Bayer, linatarajia kutumia zaidi ya Sh bilioni 1.173 katika msaada wa tani 200 ambazo ni sawa na kilo 200,000 za mbegu za mahindi aina ya Dekalb au DK na kilo 100 za mbegu za mboga zinazoitwa Semenis.

Shirika hilo linashirikiana na Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT), ambapo msaada huo unatolewa kupitia mpango wa ‘Mashamba bora. Maisha bora Tanzania’, wenye lengo la kuchangia wakulima wadogo wadogo ambao wanakabiliwa na changamoto mpya zilizotokana na janga la Covid-19.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASTA, Bob Shuma,akizindua msaada wa mbegu kwa wakulima Tanzania,uliotolewa na Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na sayansi ya kilimo katika nyanda za afya na lishe bora la Bayer,ambalo linatarajia kutumia zaidi ya Sh bilioni 1.173 kwa ajili ya tani 200 za mbegu za mahindi na kilo 100 za mbegu za mboga zitakazotolewa kwa wakulima kutoka wilaya 25 zilizopo nchini.

Akizungumza jana jijini Arusha wakati wa halfa ya uzinduzi wa mpango huo hapa nchini,Meneja wa Shirika hilo Tanzania, Frank Wenga, amesema katika mpango huo wamelenga kuwasaidia wakulima kwa kuwapa mbegu hizo, kutoa elimu ya ugani kwa kushirikiana na wadau wengine pamoja na kuwaunganisha wazalishaji na wanunuzi wa mazao kupitia mnyororo wa thamani.

Amesema mpango huo wa unaotekelezwa katika kipindi cha miaka miwili 2020-2022 umeshazinduliwa katika nchi nyingine Barani Afrika ambazo ni Kenya, Nigeria, Zambia, Malawi, Afrika Kusini na Msumbiji ambao utanufaisha wakulima laki saba  kutoka nchi zote huku kati ya hao wakulima laki moja wakiwa ni Watanzania.

Meneja huyo anasema mpango huu unaendeleza malengo ya kidunia ya Bayer ya kuwezesha wakulima wadogo milioni 100 ifikapo mwaka 2030, ili kusaidia kujikinga na baa la njaa na kuhakikishia mahitaji ya chakula yanajitosheleza.

“Pembeni yetu hapa tunaona lori lenye mbegu ambazo ni tani nane ambazo ni sawa na kilo 8,000 ambazo ndizo zitaanza kugawanya.Katika kipindi cha janga la Covid-19 shughuli za wakulima ikiwemo suala la uhakika wa chakula vipo kwenye tishio kubwa, kutetereka na kufungwa kwa biashara mbalimbali kumesababisha ugumu wa kupatikana mbegu au pembejeo,” amesema Wenga.

Amesema katika mpango huo wanatarajia kufikia wakulima wadogo laki saba na kati ya hao wakulima laki moja ni kutoka Tanzania na kuwa kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii kitawaunganisha wakulima na masoko mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Wakulima wadogo wanakumbana na changamoto kupata bidhaa zenye ubora na za kutegemewa,wanahitaji kuzalisha mazao mengi ila katika kipindi cha janga la Covid-19 shughuli za wakulima wadogo hasa suala zima la uhakika wa chakula vipo kwenye tishio kubwa.

“Kulingana na lengo letu la Afya kwa wote,Bila kujali njaa”,tumedhamiria kutoa msaada kwa wakulima wadogo ambao wanahitaji kushughulikia changamoto za sasa na kuimarisha ustahimilivu na tutashirikiana na wahisani kutengenza mipango ya muda mfupi na mrefu kujenga ustahimilivu wa mifumo ya ustahimilivu ya chakula,”amesema Wenga.

Awali, akizindua mpango huo, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya wafanyabiashara wa mbegu nchini(Tasta), Bob Shuma, amewataka wakulima hao watakaonufaika na mpango huo kuhakikisha wanazingatia na kufuata maelekezo ya maafisa ugani ili waweze kuzalisha kwa wingi na kuzingatia ubora. Aidha amesisitiza vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika kilimo.

“Nawasihi sana vijana wajitokeze kwa wingi na waonyeshe wana moyo wa dhati na kujishughulisha na kilimo na kilimo ili kikunufaishe kinahitaji ujitume na uwe na nidhamu,mtakaonufaika na mpango hui mjitume na muwe mfano wa kuigwa,”amesema Shuma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles