26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Kitanda tiba chawa kivutio banda la VETA maonesho ya Nanenane

Derick Milton, Simiyu

Wakati wa maonesho ya sikukuu ya wakulima kitaifa (Nanenane) yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu yakifikia siku ya sita leo, kituo kikubwa kimekuwa kitanda tiba kilichopo banda la Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA ).

Kitanda hicho kimekuwa kikivutia watu wengi kutaka kukiona na kupata maelezo yake, kutokana na mwonekano wake, ambapo kwa ndani kimewekewa mkaa huku kikiwa kimewekwa godoro jepesi.

Umati wa wananchi ambao wamekuwa wakitembelea maonyesho hayo, umekuwa ukikusanyika kwa wingi kwenye kitanda hicho, ambapo wengi ushangaa baada ya kuambiwa kuwa ni katanda tiba.

Mkurugenzi wa kituo cha kulea wahitimu chuo hicho Oswin Komba ambaye ndiye anahusika kutoa maelezo ya kitanda hicho, anasema kuwa watu wengi wanashangaa kusikia kuna kitanda tiba.

Komba anasema kuwa kitanda hicho ni tiba sahihi kwa watu wenye matatizo ya mgongo, kiuno na mbavu, au watu wenye matatizo ya uti wa mgongo kuweza kupona matatizo hayo.

Mbali na hilo Oswin anasema kuwa kitanda hicho kinasaidia kubadilisha hali ya hewa na kuleta hewa safi ikiwa kitawekwa kwenye chumba kidogo chenye uwezo mdogo wa kubadilisha hewa.

“Kuna watu wakienda hospitalini wakakutwa na matatizo ya mgongo wanaambiwa walale chini na siyo kwenye godoro, VETA tuliamua kutengeneza teknologia hii unalala kwenye kitanda chenye godoro lakini mgongo hauwezi kupinda unanyooka kama mtu aliyelala kwenye sakafu,” anasema Komba.

Mtaalamu huyo anasema kuwa mtu kuendelea kulala kwenye sakafu, anaweza kulala kwenye kitanda hicho na akapona kabisa tatizo la mgongo “ nah ii teknologia tunatengeneza sisi VETA”

Joshua Adamu mmoja wa wananchi alisema kuwa VETA wana ubunifu wa hali ya juu, huku akishangaa kuona kitanda tiba ambacho kwa ndani kimewekewa mkaa na kinaweza kutibu tatizo la mgongo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles