29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kimeta chaua wawili Moshi

Upendo Mosha

WATU wawili wameripotiwa kufariki Dunia kwa ugonjwa wa kimeta baada ya kudaiwa kula nyama yamzoga wa Ng’ombe,wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari leo, Februari 22, Ofisini kwake Mjini Moshi, Mkuu was mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mgwhira,alisema watu hao walifariko na kwamba wengine watano wanapatiwa matibabu katika hospital ya Rufaa ya KCMC na Kilema.

“Tumepokea taarifa watu wawili wamefariki kwa kimeta baada ya kula mzoga wa nyama ya ng’ombe…watano wanapatiwa matibabu ambapo watatu Kati yao wapo Hosptali ya KCMC na wawili Hosptali ya Kilema”alisema

Adha alisema wagonjwa hao watokea katika maeneo ya Njiapanda, Mwika na Kilema na kwamba kwa serikali tayari imeweka zuio la mifugo kutotoka katika maeneo hayo bila kibali Cha Mganga Mkuu wa wilaya hiyo.

Alisema kwasasa ugonjwa huo upo katika wilaya za Siha,Rombo na Moshi vijiji na kwamba waliofariki mazishi yao yanafanyika chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles