24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kijeba wa Congo Brazzaville aitega CAF

langa-lesse-bercyNa MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MCHEZAJI wa timu ya taifa ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 ya Congo Brazzaville, Langa-Lesse Bercy, ameshindwa kutokea mjini Cairo, Misri kwa ajili ya kufanyiwa vipimo ili kuthibitisha umri wake kwa kipimo cha  MRI (Magnetic Imaging Resonance).

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kutoridhika na kujiridhisha kuwa mmoja wa wachezaji wa Jamhuri ya Congo-Brazzaville alikiuka kanuni za mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 mwaka huu, lilimkatia rufaa mchezaji huyo katika Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

Kutokana na rufaa hiyo dhidi ya mchezaji huyo wa Congo, CAF liliagiza apelekwe Makao Makuu ya Shirikisho hilo, lililoko Cairo, Misri kwa ajili ya kurudia na kuthibitisha umri wake.

TFF iliagizwa na CAF igharimie zoezi zima, ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za usafiri wa mchezaji husika na daktari wake pamoja na kulipia gharama za vipimo ambapo TFF ilikubaliana na matakwa hayo ya CAF na kulipia.

Kipimo ilikuwa kifanyike jana saa 5.00 asubuhi mjini Cairo, Misri. Ujumbe wa TFF wa watu wanne ukiambatana na madaktari wawili uliwasili mjini Cairo tangu Novemba 17 mwaka huu, ili kuwa shuhuda wa zoezi la kipimo hicho.

Juzi usiku saa 5.00 TFF ilipokea ujumbe kutoka CAF kuwa mchezaji Langa Bercy ameshindwa kusafiri kwenda Cairo kwa kuwa yuko katika eneo lililoko vitani, eneo hilo hata hivyo halikutajwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, TFF inaendelea kufuatilia kwa karibu jambo hilo ili kuhakikisha haki inatendeka.

Kadhalika TFF inaomba wadau wa mpira wa miguu wawe na subira katika kipindi hiki.

Congo Brazzaville ilifuzu kucheza fainali za vijana kwa umri huo zitakazofanyika Madagascar mwakani, baada ya kuifunga Serengeti Boys bao 1-0 katika mechi ya marudiano iliyochezwa nchini humo.

Katika mechi ya awali iliyochezwa jijini Dar es Salaam, Serengeti Boys waliifunga timu hiyo  mabao 3-2.

Iwapo itabainika mchezaji huyo kudanganya umri, CAF inaweza kuipa Serengeti Boys nafasi ya kucheza fainali hizo.

Itakumbukwa kuwa Serengeti Boys ilifuzu kwa fainali hizo mwaka 2005 nchini Gambia, lakini ilishindwa kushiriki baada ya kutolewa na CAF  kutokana na kumchezesha ‘kijeba’ beki Nurdin Bakari, aliyekuwa pia akiitumikia klabu aya Simba wakati huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles