Na KULWA MZEE -DAR ES SALAAM
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemwachia huru aliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart), Robert Kisena (46) na wenzake watatu na kuwakamata tena, kisha wakaunganishwa na mke wa kigogo huyo, Frorencia Mshauri (43) katika kesi ya uhujumu uchumi namba 38 ya mwaka 2019.
Washtakiwa hao waliunganishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Grolia Mwenda ambaye alidai wanakabiliwa na mashtaka 19 likiwamo la kusababisha hasara ya Sh bilioni 2.4 kwa Kampuni ya Udart.
Awali washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na kesi mbili tofauti mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba na Hakimu Rwizile.
Upande wa mashtaka uliomba washtakiwa wafutiwe mashtaka chini ya kifungu cha 91 (1) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) sura ya 20 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 kwa maelezo kuwa mkurugenzi wa mashtaka hana nia ya kuendelea na kesi hizo ndipo mahakama ilidhia na kuwaachia huru.
Washtakiwa hao waliendelea …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.