28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tume ya Atomiki yawataka wafanyabiashara kuhakiki mionzi isiyo na madhara

Tume ya Nguvu ya Atomiki Tanzania (TAEC) imewataka wafanyabiashara nchini kuendelea kupima bidhaa zao ili kuhakikisha mionzi yake ni salama na haitaleta madhara.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Prof. Busagala alopowasilisha mada katika mkutano wake na baadhi ya wafanyabiashara wa jijini Mwanza ambapo amesema kuwa kupima bidhaa zao ni jambo la kufuata sheria.

Akizungumza leo, Mei 15, Jijini Mwanza Prof. Busagala amewaeleza wafanyabiashara hao juu ya majukumu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania kisheria, ili kuongeza uelewa na kujadiliana hatua mbalimbali ambazo zitaisaidia Tume hiyo ili kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara.

“Tume ya Atomiki Tanzania ni pamoja na kuangalia mapungufu mbalimbali na hatimaye kuchukua hatua stahiki ili kuweka ustawi mzuri kati ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Mwanza na wafanyabiashara wote wanaolizunguka ziwa Victoria na maeneo menginine nchini na kuyafanyia kazi kwa lengo la uboreshaji,” amesema Mkurugenzi huyo.

Kwa upande mwingine katika mkutano huo Prof. Busagala amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa athari za mionzi zinaweza kuleta madhara makubwa endapo kutakuwa na ukiukwaji wa kisheria

Pia Prof. Busagala alisisitiza kuwa umakini na ushirikiano mkubwa unahitajika ili kuendelea kudhibiti wa mionzi ili kutosababisha madhara yanayoweza kusababishwa na vimelea vya mionzi kwa wananchi na mazingira na kuna ulazima mkubwa wa kupima bidhaa hizo ili kukidhi matakwa ya sheria ya Nguvu za Atomiki (Atomic Act No 7) na Sheria za Kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles