NYOTA wa Bongo Fleva, Kassim Mganga, amesema kabla hajaanza kufanya muziki alikuwa mfanyakazi wa kupokea na kutoa mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam, lakini kipaji chake cha muziki kilimwachisha kazi hiyo kutokana na ujira mkubwa aliokuwa akipata kupitia muziki wake.
Kassim alisema kwa mwezi alikuwa akilipwa Sh 200,000 kwa kazi ya bandarini lakini katika onyesho lake moja la muziki alipata Sh 500,000 ndipo akaamua kuacha kazi ya bandari na kuendelea na muziki.
“Nilipofanya wimbo wangu wa kwanza wa ‘Haiwezekani’ nilipata shoo ya kwanza iliyoniwezesha kupata laki tano fedha ambazo ziliniongezea nguvu ya kufanya muziki kwa kuwa niliona mabadiliko makubwa kati ya kazi za watu na muziki wangu,” alieleza Kassim katika uamuzi wake huo.