Mr. Blue: Ndoa ina neema katika muziki

0
1606

Mr. Blue, mkewe na watotoNA THERESIA GASPER

MSANII wa kizazi kipya nchini, Khery Sameer ‘Mr Blue’, amewaeleza wasanii wenzake ambao hawajaolewa na wale wasiooa kwamba ndoa ina neema kubwa kimuziki hivyo watimize jambo hilo mapema.

“Inasikitisha vijana wengi wake kwa waume waliofikisha umri wa kuoa na wale wa kuolewa wanakwepa kutimiza ndoa wakihofu kupotea kimuziki lakini nawaeleza kwamba ndoa ina uhusiano mzuri na mafanikio ndiyo maana wengi waliooana wanafanya vizuri katika mambo yao,” alieleza Mr Blue.

“Nawashauri wasanii ambao muda wa kuoa umefika waoe ili wajiongezee heshima na kuzidi kukubalika katika jamii kwa kuwa ile dhana ya kuonekana wahuni itapotea na pia fursa mbalimbali na heshima dhidi yao zitafunguka,” alisema.

Msanii huyo licha ya kuoa kwa sasa anaendelea vema na muziki wake huku akiwaomba waendelee kuupenda muziki mzuri unaotolewa naye kwa ajili yao kwa kuwa amejipanga mwakani kuendelea na nyimbo nzuri kwa ajili yao huku akiendelea kuboresha ndoa yake iwe mfano wa kuigwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here