26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kariakoo ya usiku na mchana kuanza Mei-Makonda

Brighiter Masaki -Dar Es Salaam

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka wafanyabishara wa soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam, kuanza  kufanya biashara saa 24 kuanzia Mei wakati wa mwezi Ramadhani.

Alisema hayo wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) jana jijini alisema katika kuufanya mkoa huo kuwa kitovu cha uchumi, tayari mkakati ya kuifanya Kariakoo kuendesha biashara kwa saa 24 umekamilika.

Makonda aliwataka wafanyabishara kujiandaa kwa kujihakikishia ulinzi wa kutosha ili wakati utakapofika, waendeshe biashara zao bila wasiwasi.

“Kariakoo ya usiku na mchana itafungua fursa mpya za kiuchumi Dar es Salaam, napendekeza mpango huu uanze raski wakati wa mwezi Ramadhani ili ndugu zetu waanze kuhudumiwa masaa 24.

 “Mkoa wetu lazima uendele kuwa kitovu cha biashara na naendelea kusisitiza tu ufungaji wa Kamera za ulinzi,” alisema Makonda.

Awali, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge alisema katika kikao hicho, wajumbe watapokea mawasilisho ya kuboresha mfumo na mazingira ya uwekezaji.

Pia Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo, alisema wametenga  Sh bilioni 3.4 kwa ajili ya kuwakopesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika bajeti ya mwaka 2020/21.

Akiwasilisha taarifa ya wilaya hiyo, Chongolo alisema fedha hiyo itatokana na mapato ya ndani.

“Sh bilioni 1.3 itatolewa kwa wanawake, Sh bilioni 1.3 kwa vijana na Sh milioni 690.4 kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

“Na tumeweka mkakati wa kuhakikisha makundi haya yanapatiwa pesa kwa wakati na bila kero yoyote,” alisema Chongolo.

Akizungumzia mikakati ya kuongeza ukusanyaji wa mapati kwenye wilaya hiyo, Chongolo alisema wanatarajia kujenga kituo cha daladala katika eneo la Mwenge.

“Kituo hicho pia kitazungukwa na maduka mbalimbali lakini pia tutajenga uwanja wa mpira kwenye eneo hilo,” alisema Chongolo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia aliishauri kikao hicho cha kamati ya ushauri ya mkoa kutafuta takwimu za watu wenye ulemavu ili waweze kusaidiwa.

Hata hivyo, Makonda alisema hoja ya kuwa na takwimu sahihi za watu wenye ulemavu ni muhimu kwa sababu itasaidia kundi hilo kufikishiwa mahitaji muhimu ikiwamo mikopo.

“Hata hili suala la kuwaunganisha kwenye vikundi vya uchumi naona kama linawagawa kwamba walemavu watafutane, wakae pamoja ndio wapewe mikopo. Nadhani pamoja na hilo, walemavu wachanganywe kwenye makundi,” alisema Makonda.

Mkuu wa Wilaya ya Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva alisema wilaya hiyo imeanza kudhibiti madanguro na biashara ya ukahaba kwa kuandaa mahakama inayotembea (mobile cort).

Alisema kupitia mahakama hiyo watuhumiwa wakikamatwa, wanafikishwa mahakamani na kuhukumiwa wakati huo huo.

 “Vita ya madanguro na machangudoa inaendelea na nimepewa mobile court (mahakama inayotembea) machangudoa wakikamatwa wanafungwa palepale hakuna tatizo. Vita nyingine niliyo nayo ni ya wavuta bangi, hii napambana nayo pia,” alisema.

Akizungumzia elimu, Lyaniva alisema wilaya hiyo katika bajeti ya mwaka 2020/21 wamefanikiwa kutenga bajeti kwa ajili ya taulo za kike.

 “Hili nalo tumelifanya ili wale watoto ambao walikuwa hawafiki shule kwa kukosa taulo za kike waweze kupatiwa,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, alisema “Sh milioni 411 zimetolewa kwa makundi maalum ya wanawake, vijana na walemavu katika bajeti ya mwaka 2019/2020.

“Pesa hizo zilizotolewa ni za mapato ya ndani kama maelekezo yanavyosema, tutaendelea kutekeleza mpango huu kama tulivyo elekezwa,” alisema Msafiri.

Hata hivyo amefafanua kuwa katika bajeti ya mwaka 2020/21 walifanikiwa kukusanya Sh bilioni 2.2.

Wachina wakiri kumuhonga Kamishna Mkuu TRA Sh milioni 11.5

NA KULWA MZEE

DAR ES SALAAM

RAIA wa wawili wa China wamekiri kutoa rushwa ya Sh milioni 11.5 kwa Kamishna wa  Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, DK. Edwin Mhede ili awasaidie wasilipe kodi ya Sh bilioni 1.3.

Washtakiwa hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu  Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

 Wakili wa Serikali, Mwakatobe Mshana  aliwataja washtakiwa kuwa ni Zheng Rongnan (50) na Ou Ya (47) wote wakazi wa Kinyambo  Mafinga C Iringa.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili Mwakatobe alidai Februari 24, 2020 washtakiwa wote wakiwa katika Makao Makuu ya TRA yaliyopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es  Salaam walitoa rushwa ya dola za Marekani 5000 sawa na Sh milioni 11.5 za kitanzania kwa Kamishna Mkuu wa TRA Dk. Edwin Mhede kama kishwawishi awasaidie kwa kampuni yao kutolipa kodi ya Sh bilioni 1.3 kiasi ambacho kilipaswa kulipwa TRA.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa walikiri kutenda kosa hilo.

Baada ya washtakiwa kukiri Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itakuja leo kwa ajili ya maelezo ya awali lakini upande wa mashtaka umlete mkalimani kwa ajili ya mshtakiwa wa kwanza ambaye hajui kingereza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles