24.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Umeme wa Nyerere kuuzwa nchi za SADC

Faraja Masinde -Dar es Salaam

SERIKALI imesema kukamilika kwa mradi wa kufua Umeme wa maji wa Julius Nyerere katika maporomoko ya Mto Rufiji  utainufaisha Tanzania na kuipa uwezo wa kuuza nishati hiyo kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, wakati waufunguzi wa mkutano wa kamati ya nishati ya SADC kutoka nchi 12 unaolenga kuwa na nishati toshelevu.

Alisema mkutano huo utakaodumu kwa siku nne ni matokeo ya maagizo ya viongozi wa nchi waliokutana mwaka jana jijini Dar es Salaam, unalenga kuzifanya nchi hizo wanachama kuwa na nishati toshelevu.

“Lengo kubwa ni kufanya sekta ya nishati ndani ya nchi zetu iwe toshelevu na kwa wale ambao wanaweza kutoa ya kutosha kama sisi kuweza kuwauzia wenzao ambao wanaupungufu wa huduma hiyo.

“Hivyo hata sisi iwpao mradi wetu wa bwawa la Julias Nyerere utakapokamilika na tutakapokuwa na nishati ya kutosha kwa ajili ya matumizi ya ndani, itakayobaki tutweza kuiuza kwa wenzetu ambao wanaupungufu wa nishati tukafanya biashara,” alisema Zena.

Alisema kuwa kuna miradi ya kuunganisha nchi kwa nchi na kwmaba umeme ni matumizi muhimu mbali na maendeleo ya viwanda kwani utachangia kuhifadhi mazingira.

“Kwani sote tunafahamu kwamba kwa sasa kuna matumizi mengi ya nishati ikiwmao magari yanayotumia nishati, matumizi ya nyumbani na masuala mengine kwani kukiwa na huduma ya gesi au ya umeme itakuwa ni rahisi kumwambia mwananchi aache kutumia kuni atumie umeme au gesi na akakuelewa kwani hata bei itakuwa rahisi” alisema Zena.

Upande wake Kamishina wa Masuala ya Petroli na Gesi kutoka Wiazara ya Nishati, Adam Zubeiry, alisema mkutano huo uliokutanisha Wakurugenzi, Makamishna na Wataalamu, unafuatilia utekelezaji wa maamuzi ambao umefanywa na wakuu wa nchi.

“Hivyo utajadili miradi mbalimbali ambayo iko kwenye hatua tofautitofauti ikiwmao mpango wa matumizi ya gesi asilia katika nchi za SADC, hivyo huu ni maandalizi ya mapendekezo yatakayojadiliwa na mawaziri husika katika mkutano utakaofanyika Mei mwaka huu hapa nchini,” alisema Zubeiry.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles