24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kapombe bado Simba

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba, imetangaza kumwongezea mkataba wa miaka miwili zaidi, beki wake wa kulia, Shomari Kapombe, kuelekea katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.

Kapombe hakuweza kucheza kwa takribani mzunguko wa pili msimu uliopita baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu kutokana na kuu­mia enka akiwa kambini nchini Afrika Kusini na kikosi cha Taifa Stars.

Kambi hiyo ilikuwa ya ku­jiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon2019), inayoendelea nchini Misri.

Hadi sasa, Simba imeshawaongezea mikataba Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Meddie Kagere, John Bocco, Aishi Manula na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, huku ikiwajumuisha kundini wazawa wapya, Kennedy Juma kutoka Singida United na Beno Kakolanya (Yanga).

Wachezaji wa kigeni waliosaini mkataba Msimbazi hadi sasa ni Wabrazili Gerson Vieira na Wilker Henrique da Silva na Msudan, Sharaf Abdalrahman.

Licha ya Kapombe kuongezewa mkataba mpya, lakini kuna taarifa kuwa klabu hiyo imemtumia ujumbe beki wao, Zana Coulibaly, raia wa Ivory Coast kutua nchini ili kusaini mkataba mpya.

Taarifa iliyotolewa jana na mtandao wa Simba, ilisema kuwa Shomari kwa sasa yupo fiti na atakuwa sehemu ya kikosi ambacho kitakwenda nje ya nchi kujiandaa na msimu mpya.

“Beki bora wa kulia nchini, Kapombe, amesaini mkataba mpya wa miaka miwili ambao utawezesha kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha mabingwa wa Tanzania Bara,” ilieleza taarifa hiyo.

Kapombe ni mchezaji tegemeo katika kikosi hicho ambaye aliisadia Simba kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa mwaka 2017/18.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles