JB awapa somo wasanii

0
1044

Na GLORY MLAY

NGWIJI la filamu Tanzania, Jacob Steven ‘JB’ amesema ni ngumu msanii kuishi vizuri kwa kutegemea mapato yanayotokana na mauzo ya kazi zake pekee, hivyo ni lazima awe na biashara nyingine.

Msanii huyo alisema kwa maisha ya sasa ni lazima kujichanganya katika shughuli tofauti zitakazoleta maendeleo katika maisha ili soko likiyumba mambo yasiharibike.

“Sitegemei filamu pekee kwani hali ya maisha imebadilika, nina biashara zangu za hapa na pale pia nawashauri wasanii wenzangu tusitegemee filamu pekee, tufanye hata biashara ndogo ndogo basi,” alisema JB.

Msanii huyo ameonekana kuwa na hofu ya tasnia ya filamu kuja kufa kutokana na kukosa ubunifu kama ilivyo zamani, hivyo amewataka wasanii wasijisahau.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here