30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

KANGI AAGIZA KIGOGO NIDA AKAMATWE

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola

Na SARAH MOSES – DODOMA                      |                         


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemwagiza Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, kumkamata aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu.

Lugola pia ameagiza kukamatwa kwa wamiliki wa kampuni tatu zinazodaiwa kuhusika katika mradi wa vitambulisho vya taifa, Gotham’s International Limited, Gwiholoto Impex Ltd na Aste Insurance, wanaodaiwa kufanya udanganyifu na kushindwa kurejesha fedha walizotumia kinyume na utaratibu.

Licha ya hali hiyo, waziri huyo ameagiza wafanyakazi wote waliohusika na ubadhirifu wa fedha za umma kwa kuingia mikataba ya kifisadi iliyoisababishia Serikali hasara, nao wakamatwe pamoja na wakurugenzi wa makampuni ya Ms. Aste Insurance Broker Company Ltd, Sykes Travel Agent Ltd, Gotham International Ltd na DR. Shija Paul Rimoy.

Lugola alitoa agizo hilo jijini hapa jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Katika maelezo yake, alisema viongozi lazima wakamatwe kwa sababu Serikali ya awamu ya tano haitaki kuchezewa.

“Nafasi ya kula fedha za umma katika Serikali ya awamu ya tano haipo na wafanyakazi wote wa umma waelewe hilo, kwamba maeneo wanayofanyia kazi ya kupiga dili fedha za Serikali, hayaruhusiwi tena.

“Pamoja na kwamba nimetoa maagizo hayo, ieleweke kwamba katika juhudi zote tulizozifanya katika kufuatilia fedha ambazo zilikuwa zikidaiwa na NIDA kutoka kwenye makampuni kadhaa, zimeweza kurejeshwa kwa kiasi kikubwa kwani hadi sasa zaidi ya Sh bilioni 575, tumeziokoa ambazo ni sawa na asilimia 84 ya fedha tulizokuwa tukidai.

“Ili liwe fundisho kwa wengine, wamiliki wa makampuni hayo pamoja na wafanyakazi wa NIDA, wanatakiwa kukamatwa na kufikishwa kwenye Mahakama ya Mafisadi ifikapo saa 12 leo (jana) jioni.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles