25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

KAMPUNI ZA SIMU ZISIZOJISAJILI DSE KUBANWA NA SHERIA

Na JUSTIN DAMIAN


SERIKALI imesema itachukua hatua kali dhidi ya kampuni ya simu ambayo haitatekeleza agizo linayoyataka kujiorodhesha na kuuza asilimia 25 ya hisa zake katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Sheria ya Electroniki na Mawasiliano ya Posta (EPOCA)  na Sheria ya Fedha ya Mwaka 2016 inayataka makampuni yote ya simu  nchini kujiorodhesha DSE.

Makampuni yalitakiwa kuwa yamekamilisha taratibu za kujiorodhesha kufikia Desemba 31 lakini hadi sasa ni kampuni moja tu imejiorodhesha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mauzo ya hisa za Vodacom Tanzania, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji alisema Serikali haitasita kuzichukulia hatua kampuni yoyote ambayo itashindwa kutekeleza matakwa ya sheria hizo mbili.

“Serikali inayataka makampuni yote ya simu kuandaa Waraka wa Matarajio   kuweza kujiorodhesha DSE bila shuruti,” alisema.

Dk. Kijaji aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuwa ya kwanza kujiorodhesha DSE kati ya makampuni 64 yanayotakiwa kujiorodhesha.

Alisema kitendo cha makampuni kujiorodhesha yatawafanya Watanzania kuwa sehemu ya makampuni hayo na hivyo kunufaika kwa uchumi. Kujiorodhesha kutaongeza uwazi jambo ambalo litasaidia kuiongezea  serikali urahisi wa kukusanya kodi,” alisema.

Naibu waziri   alisema katika  makampuni ambayo ni walipa kodi wakubwa 10, sita wamejiorodhesha katika soko la hisa.

  Mkurugenzi Mtendaji wa   Vodacoma Tanzania, Ian Ferrao alisema kampuni yake itaendelea na lengo lake la kuwawezesha Watanzania kuwa sehemu ya mafanikio yake.

“Kuna kila sababu ya kwa nini mtu awekeze katika Vodacom. Kwanza ni kampuni kubwa ya simu kuliko zote na pili ni kampuni ambayo imekuwa na rekodi nzuri ya fedha na kwa hiyo ni sehemu salama na sahihi ya kuwekeza,” alisema.

Aliitaka Serikali kuuelimisha umma umuhimu wa kuwekeza kwenye his Watanzania wawe wa miliki wa uchumi wa nchi yao ambao unaonyesha ukuwa mzuri.

Vodacom inatarajia kukusanya   Sh bilioni 476 kwa kuuza  hisa milioni 56. Kila hisa itauzwa kwa Sh 850 na kiasi cha chini cha hisa ni hisa 100.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles