31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MGAWE APANGUA KESI NYINGINE

Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam


ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe, ameachiwa huru katika kesi ya rushwa iliyokuwa ikimkabili, na wenzake watatu. 

Washtakiwa hao wameachiwa ikiwa ni miezi takriban mitano tangu kesi hiyo ilipofikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo.

Washtakiwa hao waliachiwa huru jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kuomba kuondoa kesi hiyo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Uhandisi TPA, Bakari Kilo, Meneja wa Ununuzi TPA, Theophil Kimaro na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya DB Shapriya Ltd, Kishor Shapriya.

Wakili wa TAKUKURU, Emmanuel Jacob aliiomba mahakama  kuondoa kesi hiyo mahakamani kwa kutumia kifungu namba 98(a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).

Hakimu Simba alikubali maombi ya Jamhuri na kuwaachia huru washtakiwa wote.

Katika kesi iliyokuwa ikiwakabili, Mgawe, Kimaro na Kilo walikuwa wanadaiwa kuwa kati ya mwaka 2009 na 2012 mahali pasipojulikana, wakiwa katika nyadhifa zao, kupitia wakala wa Kampuni ya DB Shapriya Ltd waliomba rushwa ya Dola za Marekani milioni nne. 

Awali ilidaiwa  waliomba kiasi hicho cha fedha kama kishawishi cha kuiwezesha kampuni hiyo kupata zabuni ya kuweka boya la kushushia mizigo (SPM) na bomba la mafuta RAS TPA, Mji Mwema.

Shapriya alikuwa anadaiwa kati ya mwaka 2009 na 2012 alitoa rushwa kwa Mgawe, Kilo na Kimaro, ikiwa ni kishawishi cha kupata zabuni hiyo.

Washtakiwa hao waliposomewa shtaka hilo kwa mara ya kwanza walikana na upande wa Jamhuri ulidai upelelezi  haujakamilika.

Washtakiwa waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyokuwa yamewekwa na mahakama likiwamo la kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika.

Mgawe alikuwa amebakia na kesi hiyo moja ambayo jana ilifutwa baada ya kesi nyingine ya matumizi mabaya ya madaraka kutiwa hatiani na kulipa faini ya Sh milioni tano Februari mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles