31.2 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati kuishauri Serikali kupitia upya tozo za ardhi

*Ni zile zinazotoka kwenye Halmashauri

*Kushauri zianze kunufaisha Halmashauri husika

Na Clara Matimo, Mwanza

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, imesema itaishauri Serikali kupitia upya suala la tozo za ardhi ambazo zinaenda moja kwa moja serikalini zianze kuzinufaisha Halmashauri husika.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, wakijadiliana jambo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Angeline Mabula leo Machi 16, 2022 baada ya kukagua mradi wa upimaji viwanja eneo Nyafula lililopo Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza. Picha Wizara ya Ardhi.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Machi 16, 2022 jijini Mwanza na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ally Makoa, baada ya kupokea ombi hilo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mipango Miji na Ardhi Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Shukrani Kyando, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kupanga, kupima na kurasimisha ardhi unaotekelezwa katika manispaa hiyo kupitia mkopo wa  Sh bilioni 3.6 kutoka serikalini iliyopewa Desemba mwaka jana.

Kamati hiyo ipo mkoani hapa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotaribiwa na serikali katika sekta ya ardhi, mradi wa mahema matatu ya kuhudumia watalii katika kisiwa cha saa na kutembelea hifadhi ya taifa ya kisiwa hicho.

Akiwasilisha ombi hilo mbele ya kamati ya kudumu ya bunge ya ardhi maliasili na utalii, Kyando, ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Mhandisi, Apolonary Modest, amesema:

”Tunaomba katika makusanyo ya ardhi tunayokusanya sehemu ya fedha iwe inarudi kwa ajili ya kutusaidia kukusanya fedha.

“Manispaa ya Ilemela kwa miaka mitatu tumekusanya kiasi cha Sh bilioni 11 kwa hiyo tunaomba kiasi chochote kiwe kinarudi kwa ajili ya kufacilitate ukusanyaji wa mapato kwa sababu saizi tunakusanya mapato ya ardhi kwa kutumia fedha za own source ambazo unakuta halmashauri ina mambo mengi ikiwemo ujenzi wa madarasa, hospitali na  asilimia 10 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa makundi maalum,” amesema Kyando.

Akitolea ufafanuzi ombi hilo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Makoa, amesema kwa kuwa ombi hilo limetolewa katika kila halmashauri walizopita kukagua miradi ya maendeleo ya kimkakati ya sekta ya ardhi pamoja na kwamba serikali ilikwisha fanya maamuzi kupitia bunge na wao ndiyo waliopitisha watakaa nayo ili kuona jinsi gani wanaweza kulishughulikia.

“Kwa kweli kati ya halmashauri zote tulizopita Ilemela mmefanya vizuri sana katika mradi huu wa kupanga, kupima na kumilikisha wananchi ardhi maarufu kama KKK, ingekuwa natoa maamuzi mimi mwenyewe leo ombi lenu hili ningelipitisha moja kwa moja, lakini niwaahidi kwamba tutakwenda kulishughulikia pamoja na serikali,”amesema.

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza(CCM) amekiri idara ya ardhi kutotengewa fedha za kutosha kwa ajili ya kufanya kazi inayokusudiwa hivyo ili kutatua changamoto hiyo wizara yake inaandaa mwongozo  ambao utazielekeza halmashauri zinapochukua fedha wakipima na kuuza viwanja walau watenge asilimia kati ya arobaini hadi 60 zirudi kwenda kuendeleza sekta badala ya kuzitumia katika shughuli zingine.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, akiikaribisha kamati hiyo mkoani humo  na kuzungumzia miradi ya KKK amesema hali ya ulinzi na usalama ni shwari changamoto zote zinaendelea kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria, ngazi za halmashauri na mkoa zinafanya usimamizi wa kina katika kuhakikisha utatuzi wa migogoro na malalamiko mbalimbali yanayohusu sekata ya ardhi  yanafanyiwa kazi kikamilifuna kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo iliyopo lengo ni kuhakikisha wananchi wanatumia rasilimali ardhi kwa utulivu na haki.

Nikuhakikishie Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati hii,  katika sekta ya ardhi tutoe elimu kwa wananchi ili wajue kwamba unapopima eneo lako unaondokana na changamoto unapunguza migogoro ya ardhi lakini tutafikia malengo kwa kutumia ardhi zetu kujiongeze kipato ndipo  tunapima ardhi.

“Tunataka huduma zote za msingi zipatikane kwenye maeneo hayo, zikiwemo nyumba za ibada, nikuhakikishie Mwenyekiti Ilemela itakuwa ni mfano bora wa maeneo yaliyopangwa vizuri Tanzania nzima kama sio Afrika Mashariki nakuhakikishia hayo kwa sababu tunae Daktari Angeline Mabula, ukiona mahali kuna daktari tafuta data maana huyu ni msomi aliye bobea katika nyanja mbali mbali anajiamini kutatua changamoto,” amesema Mhandisi Gabriel.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles