23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

COSTECH yawanao wanahabari namna ya kuandika habari za tafiti

Safina Sarwatt,Arusha

TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imetoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kutoka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ili kuwajengea uwezo wa kuandika habari za tafiti mbalimbali zinazotolewa na wanasayansi na kuzifikisha kwa wananchi kwa lugha rahisi.

Sehemu ya Wanahabari.

Akifungua mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Tume hiyo Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Dk. Philbert Luhunga amesema mafunzo hayo ya siku nne, yatawasaidia wanahabari hao kuandika habari za sayansi teknolojia na ubunifuni kwa lugha rahisi ambayo jamii wataweza kuilewa na kuleta manufaa.

Katika mafunzo hayo yanayofanyika jijini Arusha kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha yameshirikisha waandishi wa habari pamoja watafiti kutoka vituo mbalimbali vya kitafiti nchini.

Aidha, amesema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuongeza utoaji wa habari mbalimbali za kitafiti zinazotolewa nchini na kutopewa kipaumbele kama ilivyo kwa habari zingine.

Amesema katika jamii kuna vitu vingi vinawatatiza na watafiti wamekuwa wakiandika taarifa zao za majibu ya matatizo hayo lakini wananchi hawayafahamu kutokana na lugha ngumu wanayoitumia.

Nae mwezeshaji wa mafunzo hayom, Dk. Bakari Msangi amewataka watafiti kuandika machapisho mafupi ambayo yamelenga kwenye maudhui husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles