HADIJA OMARY, LINDI
Waziri wa Nishati, Medard Kalemani amewataka wakuu wa taasisi kutenga bajeti kwa ajili ya kuunganisha umeme katika taasisi zao pindi umeme wa wakala vijijini (REA) utakapofika katika maeneo hayo.
Kalemani ameyasema hayo kwa nyakati tofauti jana alipokuwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Ng’au Halmashauri ya Ruangwa na Mpenda Halmashauri ya Matama Mkoni Lindi.
Akizungumza na wananchi hao baada ya kufanya zoezi la kuwasha umeme katika Zahanati ya Ng’au iliyopo katika Kijiji cha Nandagala na zahanati ya Mpenda katika kijiji cha Mpenda Mtama kalemani aliwataka wakandarasi wote wanaotekeleza miradi hiyo ya umeme vijijini kuyapa kipaumbele cha kwanza maeneo ya taasisi kama vile shule, zahanati, makanisa, misikiti pamoja na ofisi za Serikali ya Vijiji.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Lindi shaibu Ndemanga alisema kuwa utaratibu huo wa kuwasha umeme vijijini na hasa katika Taasisi za Mmma ni mzuri kwani umeanza kuleta tija katika wilaya yao.
Amesema umeme uliopo katika shule tisa za sekondari za halmashauri hiyo umeweza kuondoa daraja sifuri katika mitihani ya kidato cha nne na kidato cha pili katika matokea ya mwaka 2019.