23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kaka wa Minaj matatani kwa ubakaji

Jelani MinajNEW YORK, MAREKANI

KAKA wa msanii wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Nicki Minaj, Jelani Minaj, amefikishwa mahakamani nchini Marekani kwa tuhuma za kubaka msichana mwenye umri wa miaka 13.

Sio mara ya kwanza kwa Jelani kufikishwa mahakamani kwa kosa kama hilo, mwaka jana mwanzoni kijana huyo mwenye umri wa miaka 37, aliachiwa huru baada ya Nicki Minaj kumtolea dhamana kwa tuhuma kama hiyo kwa msichana mwenye umri wa miaka 12.

Inadaiwa kwamba kuna ushahidi wa kutosha kwamba kijana huyo amebaka, hivyo kuna uwezekano wa kwenda jela miaka 15 upelelezi utakapokamilika.

Hata hivyo, Jelani amekanusha juu ya taarifa hizo na ameitaka mahakama kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli juu ya jambo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles