Rhett anadai alidanganywa kutia saini na kujiunga na huduma hiyo ya moja kwa moja kwa kuwa ilikuwa njia ya pekee ya kununua albamu hiyo ya West baada ya kutia saini.
Alisema kuwa alijiunga na Tidal baada ya mwanamuziki huyo kusema albamu yake haitauzwa kwingine. Jambo hilo linaonekana kuwa la kitapeli ambapo mamilioni ya wateja wameanza kuwa na wasiwasi na huduma hiyo ya Tidal.
Inadaiwa kwamba mpango huo ungekaa sawa kwa Kanye West, angefanikiwa kupata zaidi ya dola milioni 84 kutokana na mauzo hayo.