23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

JWTZ yaombwa msamaha  

jwtzNa MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Dira Newspaper Ltd ambao ni wachapishaji wa gazeti la kila wiki la Dira ya Mtanzania, imeliomba radhi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutokana na habari iliyochapishwa na gazeti hilo toleo Na. 424 la Juni 20-26, mwaka huu iliyokuwa na kichwa cha habari ‘Kifaru cha kivita JWTZ chaibwa.’

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam juzi na kusainiwa na Meneja Utawala na Fedha wa kampuni hiyo, Musiba Esaba, habari hiyo ilichapishwa baada ya mtayarishaji wa kurasa kuipanga kwa bahati mbaya ikiwa bado uchunguzi wake haujakamilika na kuiacha nyingine iliyotakiwa ichapishwe siku hiyo.

Esaba alisema watu wengi walishtushwa na habari hiyo akiwamo Mkuu wa Kikosi cha 83 KJ cha Kiluvya mkoani Pwani, ambaye kikosi chake kilitajwa kama chanzo cha habari hiyo.

“Kwa masikitiko makubwa, uongozi wa Kampuni ya Dira Newspaper unamwomba radhi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Tanzania na jeshi lote kwa ujumla, kutokana na usumbufu walioupata kutokana na kuchapishwa kwa habari ile.

“Tunapenda JWTZ na Watanzania wote kwa ujumla wafahamu kuwa gazeti la Dira ya Mtanzania halikulenga kuchafua taswira ya JWTZ kama ambavyo baadhi ya watu walivyofikiria,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles