22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

TTCL, Huawei wazindua huduma ya 4.5G

prof-faustin-kamuzora2Na MWANDISHI WETU- DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kushirikiana na Kampuni ya Huawei, wamezindua matumizi ya huduma za teknolojia ya 4.5G hapa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora, aliipongeza TTCL kwa kufikia hatua hiyo kwa sababu inaonyesha ni kwa jinsi gani ilivyodhamiria kutoa huduma bora ya mawasiliano nchini.

“Naipongeza menejimenti na wafanyakazi wa TTCL kwa juhudi kubwa za kuleta mabadiliko ya utendaji na uwajibikaji ambao ni utekelezaji wa mwongozo wa Serikali,” alisema Profesa Kamuzora.

Awali, akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba, alisema uzinduzi wa huduma hiyo ni hatua muhimu katika sekta ya mawasiliano.

“Hili ni jambo la kupongeza kwa sababu TTCL inatekeleza mpango wa mageuzi ya kibiashara kwa sababu hatua mbalimbali zinachukuliwa katika kuboresha huduma zake ili iendelee kuwa mhimili mkuu wa mawasiliano nchini.

“Kwa kutumia huduma ya 4.5G, TTCL itaongeza ushiriki wake katika kufanikisha maendeleo ya sekta mbalimbali ambazo zote kwa pamoja zinalenga kutoa huduma bora kwa wateja wa ndani na nje ya nchi,” alisema Kindamba.

Alizitaja baadhi ya huduma zitakazonufaika na huduma za 4.5 G kuwa ni pamoja na sekta ya afya, elimu, biashara na mawasiliano serikalini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles